PEER EDUCATION

ATHARI ZA  MADAWA YA KULEVYA KWA VIJANA: 


Jamii hususani vijana wanashauriwa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya mbayo yamekuwa yakiathiri nguvu kazi ya Taifa na kuwafanya vijana wengi kuishi katika hali hatalishi na kuendelea kuilalamikia serikali kutowajali na kuwatengenezea miundombinu ya kupiga hatua kimaisha.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti VIJANA MAMBO SAFI FUONDATION iliyoko kimara Baruti jijini Dar es salaam inayojishughulisha na utoaji elimu katika utambuzi wa mambo mbalimbali yenye kujenga jamii.
Aidha Mwenyekiti (Mr. Fabian) alipokuwa akizungumza na vijana wengi wanaohudhuria mafunzo ya ujasiliamali, sanaa na michezo alisema vijana wengi walivyoathirika kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya.


Amesema vijana wengi ambao ndio tegemeo katika ujenzi wa Taifa wamejitumbukiza katika matumizi ya dawa za kulevya na hivyo kushindwa kushiriki ipasavyo katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo huku wengi wao dawa hizo zikiwatuma kushiriki katika vitendo vya uhalifu.


Bwana Fabian anasisitiza ikiwa Tanzania inaungana na mataifa mengine Duniani katika kupinga matumizi ya dawa za kulevya pia inawajibu ya kupanga mikakati kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutoa elimu katika sehemu mbalimbali juu ya athari kubwa zinazotokana na dawa za kulevya ili kila jamii hasa vijana waweze kuepukana na matumizi yake.


Amesema wapo vijana ambao wanajiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya bila kufahamu athari zake na wengine kwa kuiga wale wanaotumia hali ambayo inafanya kuongezeka kwa idadi kubwa ya vijana wanaojiingiza katika matumizi ya dawa hizo.

Akitolea mfano wa dawa za kulevya aina ya bangi (Cannabis) kitaalam inamfanya mtumiaji kukosa umakini na kushindwa kufanya vitu vinavyohitajika na uwezekano mkubwa kupata kansa na kuharibu mapafu kutokana na matumizi ya muda mrefu na hata kupelekea kuzaa vilema.


"Zipo athari nyingi kutokana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi ambayo vijana wengine wamejitumbikiza huko,lakini wapo wengine kutokana matumizi ya bangi kunawapelekea kuchanganyikiwa na kupumbaa kwa ufahamu hivyo kunahitajika elimu.


"Licha ya bangi,dawa za kulevya aina ya (Narcoticks) ambapo ndani yake kuna dawa kama Heroine,darvon,hydrocodone,codeine vijana ujiingiza kuzitumia bila kujua athari zake na pengine bila kupata elimu hivyo kuendelea kuangamiza Taifa.


"Moja ya athari ya dawa hizi ni kupoteza fahamu,kuugua ugonjwa wa kifafa na hata kifo pale utakaozidisha kipimo,sasa kama elimu haitatolewa kwa vijana kwa kuzitambua athari zake  tutapoteza vizazi vingi,"alisema Fabian.


Kutokana na gharama kubwa ambazo hutumika kurudisha hali ya kawaida ya mtumiaji wa dawa za kulevya, VIJANA MAMBO SAFI FOUNDATION kwa kushirikiana na wadau wa Mashirika mengine ya kijamii Hutoa elimu ili kuweza kuwaepusha vijana na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya. 

VIJANA MAMBO SAFI FOUNDATION analenga kuwabadili vijana kuwa na fikra chanja kupitia sanaa, mafunzo kwa jamii, uchumi na vijana, michezo, sanaa na maendeleo ya jamii kwa ujumla.

0 comments:

Post a Comment

 
Mambo Safi Group © 2014 | JM Designs