Mambo Safi Group- Waandaaji wa "UMOJA NA AMANI SUPER CUP"

Mambo Safi Group, kundi lenye maskani yake Kimara-Baruti jijini Dar Es Salaam,liliandaa ligi ya mpira wa miguu iliyojulikana kwa jina la UMOJA NA AMANI SUPER CUP. ligi hiyo ilifadhiliwa ma Wazari wa Vijana, habari utamaduni na michecho Mh. Dr. Fenella Mukangara(mb), ligi hiyo ilijumuisha jumla ya timu 32 toka jimbo la Ubungo na kushuhudia Baruti FC kuibuka kinara wa michuano hiyo.

Michuano hiyo ilileta taswiri tofauti na kuwaleta vijana pamoja toka sehemu mbalimbali maana michezo ni Afya, Amani, Mshikamano na Upendo. Umoja na Amani super Cup yalikuwa ni mashindano ya aina yake huku yakichezeshwa na marefarii bingwa. Hii inaonyesha ni jinsi gani vijama wanaweza kufanya mambo mazuri na makubwa ambayo yanaweza kuwafanya vijana wakaja pamoja, wakasahau shida zao na kuburudika pamoja huku wakipata elimu ya kujitambua, kutambua fulsa mbalimbali zitakazowasaidia kujikwamua kimaisha.

Shukrani za pekee kwa Mama Mh. Dr. Fenella Mukangara (mb), kwa kufadhili mashindano hayo ambayo kmila kijana aliyafurahia, tukishuhudia mashabili lukuki toka katika vilabu vyote 32, na kikubwa zaidi ni kwamba tangu michuano inaanza mpaka inamalizika hapakuwapo na matukio yoyote ya uvunjifu wa amani, hili ni jambo la kujivunia kwa MAMBO SAFI GROUP na vijana wote kwa ujumla, bila kuvisahau vyombo vya dola.

0 comments
 
Mambo Safi Group © 2014 | JM Designs