Mh. Dr. Fenella mukangara awa mgeni rasmi katika sherehe za 2013 IYF world Camp Tanzania

Dk.Fenella MukangaraWaziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo (Tanzania) amekua mgeni rasmi katika ufunguzi wa kambi ya vijana iliyoandaliwa na IYF katika ukumbi wa Mlimani city Dar es Salaam. Ameonge mengi kuhusu vijana, kikubwa ni changamoto zinazowakabili vijana kutoka sehemu mbalimbali.
Changamoto hizo ni pamoja na Mtazamo hasi jinsi unavyoathiri tabia za vijana, hii inaambatana na dhima ya IYF (International Youth Fellowship) isemayo "BADILISHA FIKRA".
Kambi hii itawafanya vijana wengi kubadili fikra zao na kujenga fikra chanya zitakazowaletea maendeleo, pia kambi hii imekuwa ni sehemu mahususi kwa vijana kubadilishana uzoefu, kujengeana misingi ya kuvumiliana, kkujengana na kuthubutu.
Mbele ya vijana zaidi ya 2000 waziri alitambua umuhimu wa IYF kama moja ya chombo kinachoisaidia serikari kuwafikia vijana, kama ilivyo kwa NGO's nyingine kama MAMBO SAFI GROUP.

0 comments:

Post a Comment

 
Mambo Safi Group © 2014 | JM Designs