Wadau wa mpira na wananchi wakifuatilia ligi ya Mh. Dr. Fenella Mukangara (MB)

Tazama picha hizi za wadau na wananchi wakishuhudia kandanda safi uwanya wa kimara baruti "Uoja na Amani Super Cup" jimbo la ubungo.

0 comments

Je wewe mpenda mpira? na mpenda Amani?

Hii ilikuwa si "dondo" kama vijana wasemavyo bali ni kabumbu safi iliyoonyeshwa na vijana wa Jimbo la ubungo huku jumla ya timu 32 zikimenyana. Mh. Dr. FENELLA MUKANGARA (MB) Wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo akiwa katika ligi yake ya "Umoja na Amani Super Cup" jimbo la ubungo iliyo ratibiwa na Mambo Safi Group.

0 comments

Mambo Safi Kilele cha mwenge na Nyerere day Tabora 2014

Mambo Safi Group, kikundi cha vijana wenye ushawishi mkubwa katika kuhamasisha maendeleo kwa vijana hawakuwa nyuma katika kushiriki mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2014. Hapa vijana wa MSG walikua Tabora katika kilele cha mwenge na Nyerere day 2014.

0 comments

Ziara ya Mh. James Kajugusi.

Mh. James Kajugusi, Mkurugenzi wa idara ya vijana Wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo alipotembelea MAMBO SAFI GROUP.

0 comments

Mambo Safi Group- Waandaaji wa "UMOJA NA AMANI SUPER CUP"

Mambo Safi Group, kundi lenye maskani yake Kimara-Baruti jijini Dar Es Salaam,liliandaa ligi ya mpira wa miguu iliyojulikana kwa jina la UMOJA NA AMANI SUPER CUP. ligi hiyo ilifadhiliwa ma Wazari wa Vijana, habari utamaduni na michecho Mh. Dr. Fenella Mukangara(mb), ligi hiyo ilijumuisha jumla ya timu 32 toka jimbo la Ubungo na kushuhudia Baruti FC kuibuka kinara wa michuano hiyo.

Michuano hiyo ilileta taswiri tofauti na kuwaleta vijana pamoja toka sehemu mbalimbali maana michezo ni Afya, Amani, Mshikamano na Upendo. Umoja na Amani super Cup yalikuwa ni mashindano ya aina yake huku yakichezeshwa na marefarii bingwa. Hii inaonyesha ni jinsi gani vijama wanaweza kufanya mambo mazuri na makubwa ambayo yanaweza kuwafanya vijana wakaja pamoja, wakasahau shida zao na kuburudika pamoja huku wakipata elimu ya kujitambua, kutambua fulsa mbalimbali zitakazowasaidia kujikwamua kimaisha.

Shukrani za pekee kwa Mama Mh. Dr. Fenella Mukangara (mb), kwa kufadhili mashindano hayo ambayo kmila kijana aliyafurahia, tukishuhudia mashabili lukuki toka katika vilabu vyote 32, na kikubwa zaidi ni kwamba tangu michuano inaanza mpaka inamalizika hapakuwapo na matukio yoyote ya uvunjifu wa amani, hili ni jambo la kujivunia kwa MAMBO SAFI GROUP na vijana wote kwa ujumla, bila kuvisahau vyombo vya dola.

0 comments

Athari za madawa ya kulevya kwa vijana.

ATHARI ZA  MADAWA YA KULEVYA KWA VIJANA: 

Jamii hususani vijana wanashauriwa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya mbayo yamekuwa yakiathiri nguvu kazi ya Taifa na kuwafanya vijana wengi kuishi katika hali hatalishi na kuendelea kuilalamikia serikali kutowajali na kuwatengenezea miundombinu ya kupiga hatua kimaisha.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti VIJANA MAMBO SAFI FUONDATION iliyoko kimara Baruti jijini Dar es salaam inayojishughulisha na utoaji elimu katika utambuzi wa mambo mbalimbali yenye kujenga jamii.
Aidha Mwenyekiti (Mr. Fabian) alipokuwa akizungumza na vijana wengi wanaohudhuria mafunzo ya ujasiliamali, sanaa na michezo alisema vijana wengi walivyoathirika kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya.


Amesema vijana wengi ambao ndio tegemeo katika ujenzi wa Taifa wamejitumbukiza katika matumizi ya dawa za kulevya na hivyo kushindwa kushiriki ipasavyo katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo huku wengi wao dawa hizo zikiwatuma kushiriki katika vitendo vya uhalifu.


Bwana Fabian anasisitiza ikiwa Tanzania inaungana na mataifa mengine Duniani katika kupinga matumizi ya dawa za kulevya pia inawajibu ya kupanga mikakati kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutoa elimu katika sehemu mbalimbali juu ya athari kubwa zinazotokana na dawa za kulevya ili kila jamii hasa vijana waweze kuepukana na matumizi yake.


Amesema wapo vijana ambao wanajiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya bila kufahamu athari zake na wengine kwa kuiga wale wanaotumia hali ambayo inafanya kuongezeka kwa idadi kubwa ya vijana wanaojiingiza katika matumizi ya dawa hizo.

Akitolea mfano wa dawa za kulevya aina ya bangi (Cannabis) kitaalam inamfanya mtumiaji kukosa umakini na kushindwa kufanya vitu vinavyohitajika na uwezekano mkubwa kupata kansa na kuharibu mapafu kutokana na matumizi ya muda mrefu na hata kupelekea kuzaa vilema.


"Zipo athari nyingi kutokana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi ambayo vijana wengine wamejitumbikiza huko,lakini wapo wengine kutokana matumizi ya bangi kunawapelekea kuchanganyikiwa na kupumbaa kwa ufahamu hivyo kunahitajika elimu.


"Licha ya bangi,dawa za kulevya aina ya (Narcoticks) ambapo ndani yake kuna dawa kama Heroine,darvon,hydrocodone,codeine vijana ujiingiza kuzitumia bila kujua athari zake na pengine bila kupata elimu hivyo kuendelea kuangamiza Taifa.


"Moja ya athari ya dawa hizi ni kupoteza fahamu,kuugua ugonjwa wa kifafa na hata kifo pale utakaozidisha kipimo,sasa kama elimu haitatolewa kwa vijana kwa kuzitambua athari zake  tutapoteza vizazi vingi,"alisema Fabian.


Kutokana na gharama kubwa ambazo hutumika kurudisha hali ya kawaida ya mtumiaji wa dawa za kulevya, VIJANA MAMBO SAFI FOUNDATION kwa kushirikiana na wadau wa Mashirika mengine ya kijamii Hutoa elimu ili kuweza kuwaepusha vijana na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya. 

VIJANA MAMBO SAFI FOUNDATION analenga kuwabadili vijana kuwa na fikra chanja kupitia sanaa, mafunzo kwa jamii, uchumi na vijana, michezo, sanaa na maendeleo ya jamii kwa ujumla.

0 comments

Matokeo ya Ualimu ngazi ya cheti 2013 haya hapa!

Baraza la taifa la mitihani latangaza rasmi matokeo ya ualimu 2013, bofya link zifuatazo kuyaona matokeo hayo:-

GATCE 2013

GATSCCE 2013

DSEE 2013

DTE 2013

0 comments

Mh. Dr. Fenella mukangara awa mgeni rasmi katika sherehe za 2013 IYF world Camp Tanzania

Dk.Fenella MukangaraWaziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo (Tanzania) amekua mgeni rasmi katika ufunguzi wa kambi ya vijana iliyoandaliwa na IYF katika ukumbi wa Mlimani city Dar es Salaam. Ameonge mengi kuhusu vijana, kikubwa ni changamoto zinazowakabili vijana kutoka sehemu mbalimbali.
Changamoto hizo ni pamoja na Mtazamo hasi jinsi unavyoathiri tabia za vijana, hii inaambatana na dhima ya IYF (International Youth Fellowship) isemayo "BADILISHA FIKRA".
Kambi hii itawafanya vijana wengi kubadili fikra zao na kujenga fikra chanya zitakazowaletea maendeleo, pia kambi hii imekuwa ni sehemu mahususi kwa vijana kubadilishana uzoefu, kujengeana misingi ya kuvumiliana, kkujengana na kuthubutu.
Mbele ya vijana zaidi ya 2000 waziri alitambua umuhimu wa IYF kama moja ya chombo kinachoisaidia serikari kuwafikia vijana, kama ilivyo kwa NGO's nyingine kama MAMBO SAFI GROUP.

0 comments

TAARIFA YA KONGAMANO LILILOFANYIKA TAR 31,JAN 2013


Mambo Safi Group tarehe 31/07/2013 tulikutanisha vijana na wakina mama 400 katika jimbo na Ubungo kuongelea maendeleo katika Nyanja mbalimbali za Ujasiriamali michezo na sanaa. Mgeni rasmi alikuwa Mh. LYIMO (MNEC) Wilaya ya Kinondoni Mambo Safi Group kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu jimbo la Ubungo vijana wa timu shiriki wa tutakutana kesho tarehe 09/02/2013 katika ukumbi wa darajani pub saa 4.00 asubuhi kupanga makakati ya ligi hiyo inayotarajiwa kuanza hivi Karibuni.

0 comments

MH. KOKA KUTEMBELEA MAMBO SAFI GROUP

“MAMBO SAFI GROUP” tarehe 06/01/2013 tutatembelewa na Mh. Koka mbunge wa jimbo la kibaha mjini atakaeambatana na mama Serina Koka na viongozi wengine wapatao watano kimara Baruti Dar Es Salaam. “MAMBO SAFI GROUP” tupo katika maandalizi ya kupokea viongozi wa ngazi ya kitaifa na kata ya Kimara hapo tarehe 31/01/2013, lengo ni kuona shughuli zinazo tekelezwa na MAMBO SAFI GROUP. Pia kuongea na vijana na akina mama wapatao mia nne (400) katika masuala ya maendeleo ya ujasiliamali, michezo na sanaa. Mafunzo enedelevu ya ujasiliamali, Jinsia, Michezo, Sanaa na Afya, utalii na Afya, Tamaduni na kuanzisha mkakati ambao utalete tija katika jamii. Mratibu wa Ukimwi manispaa ya Kinondoni ameitimisha mafunzo ya kwanza ya Ujasiliamali kwa akina mama Wajane wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, hii ni kutokana na mafunzo endelevu yanayotolewa na “MAMBO SAFI GROUP”

0 comments
 
Mambo Safi Group © 2014 | JM Designs