ATHARI ZA MADAWA YA KULEVYA KWA VIJANA:
Jamii hususani vijana wanashauriwa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya mbayo yamekuwa yakiathiri nguvu kazi ya Taifa na kuwafanya vijana wengi kuishi katika hali hatalishi na kuendelea kuilalamikia serikali kutowajali na kuwatengenezea miundombinu ya kupiga hatua kimaisha.
Rai
hiyo imetolewa na Mwenyekiti VIJANA MAMBO SAFI FUONDATION iliyoko kimara Baruti jijini Dar es salaam inayojishughulisha na utoaji elimu katika utambuzi wa mambo mbalimbali
yenye kujenga jamii.
Aidha Mwenyekiti (Mr. Fabian) alipokuwa akizungumza na vijana wengi wanaohudhuria mafunzo ya ujasiliamali, sanaa na michezo alisema vijana wengi walivyoathirika kutokana na matumizi ya
madawa ya kulevya.
Amesema
vijana wengi ambao ndio tegemeo katika ujenzi wa Taifa wamejitumbukiza
katika matumizi ya dawa za kulevya na hivyo kushindwa kushiriki ipasavyo
katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo huku wengi wao
dawa hizo zikiwatuma kushiriki katika vitendo vya uhalifu.
Bwana Fabian anasisitiza ikiwa Tanzania inaungana na mataifa mengine Duniani katika
kupinga matumizi ya dawa za kulevya pia inawajibu ya kupanga mikakati
kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutoa elimu
katika sehemu mbalimbali juu ya athari kubwa zinazotokana na dawa za
kulevya ili kila jamii hasa vijana waweze kuepukana na matumizi yake.
Amesema
wapo vijana ambao wanajiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya bila
kufahamu athari zake na wengine kwa kuiga wale wanaotumia hali ambayo
inafanya kuongezeka kwa idadi kubwa ya vijana wanaojiingiza katika
matumizi ya dawa hizo.
Akitolea
mfano wa dawa za kulevya aina ya bangi (Cannabis) kitaalam inamfanya
mtumiaji kukosa umakini na kushindwa kufanya vitu vinavyohitajika na
uwezekano mkubwa kupata kansa na kuharibu mapafu kutokana na matumizi ya
muda mrefu na hata kupelekea kuzaa vilema.
"Zipo
athari nyingi kutokana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi
ambayo vijana wengine wamejitumbikiza huko,lakini wapo wengine kutokana
matumizi ya bangi kunawapelekea kuchanganyikiwa na kupumbaa kwa ufahamu
hivyo kunahitajika elimu.
"Licha ya bangi,dawa za kulevya aina ya (Narcoticks) ambapo ndani yake
kuna dawa kama Heroine,darvon,hydrocodone,codeine vijana ujiingiza
kuzitumia bila kujua athari zake na pengine bila kupata elimu hivyo
kuendelea kuangamiza Taifa.
"Moja
ya athari ya dawa hizi ni kupoteza fahamu,kuugua ugonjwa wa kifafa na
hata kifo pale utakaozidisha kipimo,sasa kama elimu haitatolewa kwa
vijana kwa kuzitambua athari zake tutapoteza vizazi vingi,"alisema Fabian.
Kutokana na gharama kubwa ambazo hutumika kurudisha hali ya kawaida ya
mtumiaji wa dawa za kulevya, VIJANA MAMBO SAFI FOUNDATION kwa
kushirikiana na wadau wa Mashirika mengine ya kijamii Hutoa
elimu ili kuweza kuwaepusha vijana na kujiingiza katika matumizi ya dawa
za kulevya.
VIJANA MAMBO SAFI FOUNDATION analenga kuwabadili vijana kuwa na fikra chanja kupitia sanaa, mafunzo kwa jamii, uchumi na vijana, michezo, sanaa na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment